Luke 18:31-34

31 aIsa akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa. 32 bKwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua. 33 cNaye siku ya tatu atafufuka.”

34 dWanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Isa alikuwa anazungumzia nini.

Isa Amponya Kipofu Karibu Na Yeriko

(Mathayo 20:29-34; Marko 10:46-52)

Copyright information for SwhKC